- This event has passed.
Kugawa miti 2
February 10
Tumegawa tabora
Akigawa miche hiyo Afisa maendeleo wa kata ya Tinde Bi. Eva Mlowe amesema serikali inatambua mchango unaofanywa na mashirika yasiyoyakiserikali kwa lengo la kutatua changamoto zinazoikabili jamii.
Afisa maendeleo amepongeza juhudi za shirika la Compass Tanzania kwa kuendelea kuunga mkono maono ya serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika utunzaji wa mazingira.
“Shirika la Compass Tanzania nimekuja wakati muafaka tunajivunia uwepo wa shirika hili katika kata ya Tinde kwa sababu ninaenda sambamba na sera ya Nchi kwa kweli wanamuunga mkono Mama Samia kwa kuifanya Tanzania kuwa ya kijani kwa kutunza mazingira”.amesema Afisa maendeleo Bi. Eva Mlowa
Mtendaji wa kata ya Nsalala Paul Kulwa amelishukuru shirika la Compass kwa kutoa miche ya miti mia mbili (200) ambayo waliomba ili wapande katika mazingira ya kata hiyo huku akiahidi kuilinda ili iweze kustawi vizuri.
Kata ya Nsalala miti hiyo itapandwa katika shule ya msingi Nshishinulu, Zahanati mpya ya Nshishinulu pamoja na ofisi ya kata ya Nsalala.
Aidha kata ya Itwangi miche hiyo itapandwa shule ya sekondari Imenya pamoja na Zahanati ya Butini iliyopo kata ya Itwangi Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.
Kwa upande wake meneja miradi wa shirika la Compass Tanzania Bwana Boniface Mhana amesisitiza juu ya utunzaji wa miti hiyo huku akiahidi